Meneja wa klabu ya Newcastle Rafael Benitez anakaribia kumnasa mshambuliaji wa Stoke City Joselu.

Press Association Sport wameeleza kuwa, Joselu kwa sasa anafanya mazungumzo binafsi na uongozi wa klabu ya Newcastle Utd, huku ada yake ya usajili ikitajwa kuwa Pauni milioni 5.

Newcastle Utd walionyesha nia kumsajili mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania mwenye umri wa miaka 27, majuma kadhaa yaliyopita na shinikizo kubwa lilitoka kwa Rafael Benitez.

Joselu, alijiunga na Stoke City kwa Pauni milioni 5.75 akitokea Hannover ya Ujerumani Juni 2015, na ameifungia mabao mnne katika michezo 27 aliyocheza katika msimu wake wa kwanza, kabla ya kutimkia Deportivo la Coruna, kwa mkopo msimu uliopita.

Benitez anatarajia kumsajili Joselu kwa lengo la kukiongezea nguvu kikosi chake ambacho jana kilianza vibaya kampeni za kuwania ubingwa wa ligi ya England kwa kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Tottenham.

Drake, Future washtakiwa na mwanamke aliyebakwa kwenye tamasha lao
TFF Yatuma salamu za rambirambi msiba wa Chabanga