Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu, ana matumaini makubwa ya kuona washambuliaji wa klabu hiyo Lionel Messi na Luis Suarez wakisaini mikataba mipya.

Bartomeu amesema wawili hao wapo katika mazingira mazuri ya kukamilisha mpango wa kusaini mikataba mpya, ili kuepusha hofu ambayo imetanda miongoni mwa mashabiki wa FC Barcelona ulimwenguni kote.

Kuhusu Messi, rais huyo amesem: “Messi ni mchezaji bora duniani na siku zote tunapenda kuona anakua bora dhidi ya wapinzani wake, tutahakikisha anatimiza wajibu wake akiwa hapa na wakati wowote atasaini mkataba mpya.

“Natambua kuna mashabiki wengi wameingia wasiwasi kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji huyu, hata mimi ninataka kuona suala hilo likitimia, lakini niwatoe hofu wale wote ambao wanadhani jambo hili halitofanikiwa kwa kusema kila kitu kipo kwenye mazingira mazuri”.

Kwa upande wa suala la Suarez, Bartomeu aliongeza kuwa: “Luis Suárez ataendelea kuwa na sisi, na wakati wowote kuanzia sasa atasaini mkataba mpya, kuna nafasi kubwa sana ya jambo hilo kukamilishwa kutokana na uwezo na kujituma kwake tangu tulipomsajili akitokea Liverpool miaka miwili iliyopita.

FIFA Kumpeleka Julian Draxler Santiago Bernabeu?
Mwandishi wa Dar24 akamatwa kwa habari ya ‘DC wa Ludewa kukanusha uzushi’