Hatimae uongozi wa klabu ya Simba, umemtangaza rasmi kocha Joseph Omog, kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Rais wa klabu ya Simba Evans Elieza Aveva amemtangaza kocha huyo kutoka nchini Cameroon pamoja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili ambao unamuwezesha kukinoa kikosi cha Wekundu Wa MSimbazi hadi mwaka 2018.

Omog amesaini mkataba huo leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari.

Omog amesema anaujua ukubwa wa Simba na changamoto zake na amesisitiza atapambana kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ingawa amesisitiza suala la muda kwa kuwa kila kitu hakiwezi kubadilika siku moja.

Ronaldo de Lima Aeleza Hisia Zake Kuhusu Lionel Messi
Yamoto Band Hawakuona Umuhimu Wangu kwenye Video ya Su -Rubby