Uongozi wa klabu ya Simba, hii leo unatarajiwa kumtangaza Kocha Joseph Omog katika mkutano na waandishi wa habari, baada ya kukamika kwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili.

Taarifa kutoka idara ya habari na mawasilino ya klabu ya Simba zinaeleza kwamba, hafla ya kumtangaza kocha huyo kutoka nchini Cameroon imepangwa kufanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regency.

Kocha Joseph Omog

Omog ambaye aliyeipa ubingwa Azam FC mwaka 2014, aliwasili jijini Dar es salaam mishale ya saa tisa usiku wa kuamkia hii leo, na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa klabu ya Simba.

Omog anatarajia kuanza kuinoa Simba rasmi ndani ya siku tatu ikiwa ni baada ya kuingia mkataba leo.

Video: Tundu Lissu amepata dhamana, haya hapa aliyoyaongea
Chelsea Yawatema Rasmi Falcao, Pato Na Amelia