Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joshua Nassari amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nassari amepokewa na viongozi wa CCM Mkoa wa Arusha leo, Julai 8, 2020 na kueleza kuwa amechukua uamuzi huo ili kujiunga na upande uliojikita katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema kuwa Serikali ya CCM imefanya mambo mengi makubwa katika awamu hii ikiwa ni pamoja na kuboresha elimu, huduma za vifaa vya ujenzi na miundombinu na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati.

“Wengi wanauliza kwanini niko hapa, wengine wanauliza kuhusu ubunge, sijatangaza nia sehemu yoyote,” amesema Nassari.

Nassari alivuliwa ubunge Machi 2019, baada ya kuvunja kanuni za bunge na kukosa sifa za kuwa mbunge kwa kutohudhuria mikutano mitatu bila kupewa ruhusa sa Spika wa Bunge.

Singida Utd kupambana hadi mwisho

Kocha Sven, Bocco waahidi shangwe Simba SC

Picha: Angalia taji la VPL 2019-20
Kocha Sven, Bocco wawaahidi jambo wana Simba SC