Muigizaji maarufu nchini Salome Nonge aliyefahamika zaidi kama Mama Abdul amefariki dunia baaada ya kuugua ugonjwa wa ini kwa muda mrefu.

Mugizaji huyo alifariki jana akiwa nyumbani kwake maeneo ya Mburahati jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya msiba huo ilitolewa na Masoud Kaftany, Afisa Habari wa Chama cha Waigizaji wilaya ya Kinondoni.

Wasanii mbalimbali wamemlilia Mama Abdul akiwemo Joti ambaye ameandika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiambatisha picha inayowaonesha wakiwa kazini.

”R.I.P Mama Abdull Mimi mwanao Sina cha kuongea zaidi ya kukuombea upate mwanga wa milele, Pumzika kwa amani mama..??” Joti ameandika.

Mama Abdul alijipatia umaarufu kupitia igizo la ‘Mambo Hayo’ ambalo lilirushwa kupitia kituo cha ITV mwanzoni mwa mwaka 2000.

Kadhalika, ameshiriki katika tamthilia mabalimbali kama ‘Kanitangaze’. Hadi anafikwa na umauti, tamthilia ya ‘Mwantumu’ inayorushwa kupitia DSTV ambayo ameshiriki ni kati ya kazi zake za hivi karibuni zinazoendelea kuoneshwa kwenye kituo cha runinga.

Ushoga, usagaji shule za Tanga wamshtua Mahiza, akemea
Jay Z, Meek Mill kuwachomoa jela Wamarekani Weusi