Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Ardhi, William Lukuvi kumsimamisha kazi Kamshina wa Ardhi Kanda ya ziwa, aliyemtaja kwa jina la Chawio kwa kosa la kushindwa kushughulikia mgogoro wa ardhi kati ya tajiri mmoja na bibi kizee aitwaye Nyasasi Masike huko Bunda.

Ametoa agizo hilo kwa njia ya simu baada ya kukutana na kero hiyo wilayani Bunda mkoani Mara alipokuwa akiendelea na ziara yake mkoani humo.

Aidha, Lukuvi amesema kuwa anatambua uwepo wa mgogoro huo na kumwambia Rais kuwa alishatoa maagizo kwa kamishna wa ardhi kanda hiyo na mkuu wa wilaya pamoja na mkoa huo kwa pamoja washughulikie suala hilo.

”Kama ulishatoa maagizo na hajayafanyia kazi huyo kamishna kashindwa kukuheshimu anatakiwa apishe, msimamishe mara moja apishe tuchunguze suala hili la wazee hawa kudhurumiwa viwanja vyao”, amesema Rais Dkt. Magufuli

Awali Bibi huyo (Nyasasi Masike) alimueleza Rais Magufuli kuwa alimuuzia tajiri mmoja eneo la kiwanja chake kwaajili ya kupata fedha ya matibabu na baada ya kupona alikuta kajimilikisha eneo lililokuwa limebaki hivyo kukosa haki yake.

Hata hivyo, Rais Dkt. amempatia shilingi laki tano bibi Nyasasi Masike kwaajili ya matumizi yake ya kila siku. Pia Waziri Lukuvi ameahidi kuanzia wiki ijayo atakuwa wilayani Bunda kushughulikia suala hilo na amemwahidi Rais bibi huyo atapata haki yake

Video: Ona Rais huyu anavyolindwa vikali, sababu zatajwa
Pius Msekwa apongeza juhudi za Rais Magufuli