Mti wa Mbuyu uliopo Chamwino, Dodoma ambao Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa anakaa akifika Chamwino utafanywa moja ya Makumbusho ya Taifa.

Rais Magufuli amebainisha hilo leo Julai 22, 2020 alipokuwa anazindua majengo ya TAKUKURU yaliyojengwa Chamwino Dodoma.

Pamoja na hilo Rais ameahidi kuzungushia uzio shamba la Mwalimu Nyerere lililoko eneo hilo kwa ajili ya familia ya Mwalimu.

Aidha, amewaachia Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kupeleka pendekezo kwa Tume ya Uchaguzi kuhusu kubadili jina la Jimbo hilo ambapo yeye anapendekeza liitwe Chamwino badala ya Chilowa.

Sikukuu ya Eid El- Adh'haa kufanyika Ijumaa
Barnett: Gareth Bale haondoki Real Madrid