Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika ya Nyumba la Taifa (NHC).

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Sophia Kongela alikuwa mhadhiri chuo kikuu cha Ardhi (ARU).

Wakati rais Magufuli akifanya uteuzi huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemteua Dkt. Maulid Banyani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC).

Aidha, kabla ya uteuzi huo Dkt. Banyani alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi.

Mashabiki 60,000 kushuhudia Al Ahy Vs Esperance
Angela Merkel atangaza kuachia ngazi 2021