Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua, Onorius John Njole kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria (Chief Parliamentary Draftsman – CPD).

Uteuzi huo umeanza rasmi leo ambapo kabla ya hapo, Njole alikuwa Mkurugenzi wa Sheria na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Udhibiti wa Mifuko wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Aidha, Njole anachukua nafasi ya Sara Barahomoka ambaye anastaafu.

Uchaguzi Malawi: Mutharika apigwa chini Urais na Upinzani
Waziri Kalemani awataka wananchi kutunza miundo mbinu ya Umeme

Comments

comments