Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, John Kijazi amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kuanzia tarehe 22 Machi, 2018.Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) – Taaluma na Utafiti.

Pia Rais Dkt. Magufuli amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 Machi, 2018. Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Bw. Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo – Sokoine (SUA).

Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwa kuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Makinda awavaa Madiwani wanawake, awataka wajenge hoja zenye ushawishi
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 24, 2018