Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Athumani Selemani Mbuttuka  kuwa wa Msajili wa Hazina.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa. Mbuttuka utaanza leo Juni 6, 2018.

Aidha, kabla ya uteuzi huo, Mbuttuka alikuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Taifa (DAG) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali  (NAOT).

Hata hivyo, Mbuttuka anachukua nafasi ya Dkt. Oswald Mashindano ambaye tayari amekwisha staaafu.

 

Msanii Sam wa Ukweli afariki dunia
Video: Billnass afunguka sababu za kutolewa kwenye 'POCHI NENE' ya Rayvanny

Comments

comments