Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Dkt. Lutengano Undule Mwakahesya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency – PBPA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Mwakahesya umeanza tarehe 21, Novemba 2018.

Dkt. Mwakahesya aliwahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) mwaka 2016.

Serikali kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Takwimu
Niliamua kukaa kimya kwa muda wa miaka mitatu- Ester Bulaya