Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi na Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority (DSFA).

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mchenga umeanza Desemba 1,2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.

Wakati huo huo rais Magufuli amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bahari Kuu (DSFA), uteuzi wa Dkt. Sweke ulianza Desemba 1,2018 ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi( Tanzania Livestock Research Institute TAFIRI) mkoani Kigoma

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua  Dkt. Sebastian Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Bodi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) uteuzi huo ulianza Januari 26, 2019.

Pia rais Magufuli amemteua Profesa Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania( Geological Surveyor of Tanzania GST) uteuzi huo umeanza Januari 18, 2019.

Tanzania na Rwanda zapeta vita dhidi ya ufisadi
Mahakama yamfungia mipaka na benki mpinzani wa Maduro