Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi mwingine na kumteua Titus Mwinuka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
 
Ambapo kabla ya uteuzi huu, Titus Mwinuka alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
 
Mnamo Januari 1, 2018 Rais JPM alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la umeme (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba na kumteua Dk Tito Esau Mwinuka kuwa kaimu Mkurugenzi wa shirika  hilo.
Kwa mwaka 2018 Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alikuwa mfanyakazi wa kwanza kutumbuliwa na Rais John Pombe Magufuli.

Hatma ya kifuta jasho wenye vyeti feki kubainika machi
Majaliwa asimamisha uuzaji wa mali za KNCU