Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amefanaya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na  na Mkuu wa Mkoa mmoja  na pia kufanya mabadiliko  katika Wizara na Mikoa.

Taarifa iliyotolewa kutoka Ikulu na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa kwa vyombo vya habari imesema katika mabadiliko, Rais  Dkt. Magufuli  amemteua Profesa Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais, ambapo Kabla ya uteuzi huo Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,

Aidha Rais Magufuli amemteua Mhandisi  Methew  Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Florence Turuka  ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Turuka alikuwa Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa anashughulikia kilimo, ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

Rais Magufuli pia amemteua Dk. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia mawasiliano, Dk. Maria anachukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Profesa Kamuzora, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambapo Angelina anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. maria aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia mawasiliano

Aidha, Rais Magufuli amemteua Aloyce Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati huohuo Rais Magufuli amemteua Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ambapo anachukua nafasi ya Rehema Nchimbi ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida .

Rehema anachukua nafasi ya Methew Mtigumwe aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughhulikia kilimo.

Magufuli amemteua Dk. Oswald Mashindao kuwa Msajili wa Hazina ambapo anachukua nafasi ya Laurence Mafuru ambaye atapangiwa nafasi nyingine.

Makunga: Wanahabari sheria mpya isiwatishe
Wamachinga waanza kurudisha vibanda vyao