Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

Aidha, taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema kuwa uteuzi huo umeanza leo tarehe 6/ 9/ 2018 ambapo kabla ya uteuzi huo Diwani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Kamishna Diwani Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa wa Polisi, Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

 

Video: Kishindo cha JPM, Makonda achokwa, hakuna Dar ya Makonda
Video: Hata waje wabunge 100 wa CCM hawaniwezi, nitawanyoosha tu- Lowassa