Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Michael Wilfred Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ng’umbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania – OUT).

Aidha, taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kupitia, Gerson Msigwa imeeleza kwamba, Dkt. Ng’umbi amechukua nafasi ya Dkt. Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua. Jaji Stephen Mrimi Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal – FCT)

Jaji Magoiga amechukua nafasi ya Jaji Barke Mbaraka Sahel ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 19 Februari, 2019.

Walimu wajitolea kujenga darasa
Brexit: Wabunge watatu wa chama tawala wajiuzulu

Comments

comments