Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka, Wakili Mkuu wa serikali na Naibu Wakili Mkuu wa serikali.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli amefafanua kuwa amefanya uteuzi huo wa Majaji wa Mahakama Kuu kwa lengo la kujaza nafasi za Majaji waliostaafu na amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa serikali na Naibu wake kwa lengo la kuhakikisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Mkuu wa serikali zinafanya kazi vizuri zaidi katika kushughulikia masuala ya Mahakama.

Mwanasiasa mkongwe nchini Kenya afariki dunia
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 16, 2018

Comments

comments