Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, John Kijazi imesema kuwa uteuzi huo wa Prof. Jairo unaanza leo Aprili 11, 2018.

Aidha, Prof. Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika.

Young Africans yashikwa Dar es salaam
Zuckerberg aliomba radhi bunge la Marekani