Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kwa kusimamia ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Kibamba -Kisarawe.

Ametoa pongezi hiyo leo, Juni 28, 2020 wakati akizindua mradi huo wilayani Kisarawe wenye thamani ya sh. Bilioni 20.649, na kuweka jiwe la msingi awamu ya pili ya mradi Kisarawe – Pugu utakao gharimu Sh. Bilioni 7.34.

Mradi huo unajengwa na mkandarasi wa kampuni ya M/S CHICO ya China na kusimamiwa na WAPCOS Limited ya India, Tenki lililojengwa linauwezo wa kuhifadhi maji ya lita milioni 6.0 kwa siku (sawa na mita za ujazo 6,000).

Hadisasa takribani wateja 1,650 wameunganishiwa maji na maeneo ambayo yatanufaika kwa wilaya ya Kisarawe ni, kata za Kisarawe, Kazimzumbwi, Kiluvya, Kwembe, Kisopwe, Mloganzila na maeneo maalumu yenye viwanda.

Ikumbukwe kuwa chimbuko la mradi huo ni agizo la Rais Magufuli alilolitoa Juni 21, 2017 alipokuwa anazindua mtambo wa maji wa Ruvu Juu.

Awamu ya pili ya mradi huo utakuwa Kisarawe – Pugu kwa gharama ya sh. Bilioni 7.3 ambao unatarajiwa kusambaza maji katika maeneo ya Pugu, Majohe, Gongolamboto, Bangulo, Ukonga – Airwing, Kigogo na sehemu ya Kinyamwezi na Buyuni / Chanika na baadhi ya maeneo ya Kinyerezi – Tabata.

Maalim Seif atangaza nia kugombea urais Zanzibar
Habari picha: Rais Magufuli akizindua mradi wa maji Kisarawe