Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Sheria na Katiba kushughulikia kwa haraka kibali cha ajira ya watu 200 alichokitoa mwaka jana na kuwataka kurekebisha kasoro ya kutokufuatilia kwa umakini maswala ya Wizara hiyo.

Ametoa agizo hilo leo Februari 2, 2021 Jijini Dodoma  wakati wa uapisho wa Jaji Zephrine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania aliyempandika jana katika sherehe za  maadhimisho ya siku ya sheria na miaka 100 ya Mahakama Kuu nchini, kutokana na  ujasiri wa matumizi ya lugha ya kiswahili katika hukumu ya kesi ya mahakamani.

Rais Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya watu huwa  wanakosoa juhudi za kiswahili kutumika wakidai kuwa kina uhaba wa misamiati, kauli ambayo ameipinga na kusema kiswahili kina misamiati ya kutosha na ni cha 10 kwa kuzungumzwa duniani lakini pia ni lugha inayotumiwa hata kwenye vyombo vya habari vikubwa ikiwemo Televisheni ya Taifa TBC, BBC na DW.

Amesema, ”Wakati umefika sasa wa kufanya mabadiliko kwa kuwa sheria si kitu ambacho hakiwezi kubadilika, tumeshindwa kutumia kiswahili sababu ya kukosa ujasiri na utashi na kupenda vitu vya nje.”

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba amesema kuwa ameongea na Mwanasheria Mkuu kuweza kuangalia namna ya kubadili vipengele vya sheria kwenda lugha ya kiswahili.

Kumbe Simba SC walitaka kumsajili Fiston wa Young Africans
Simba SC kuifuata Dodoma Jiji, kutinga bungeni