Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli leo amekutana na wabunge wa chama hicho tawala jijini Dodoma.

Rais Magufuli ambaye alikuwa jijini humo tangu juzi, ameshiriki chakula cha mchana na wabunge hao na kuteta nao, kwa mujibu wa Katibu wa wabunge wa chama hicho, Jason Rweikiza.

“Amewaalika wabunge wa CCM leo mchana kula chakula, tumesalimiana na kupeana hongera ya kazi,” Mwananchi wanamkariri Rweikiza.

Kwa mujibu wa Rweikiza, mkutano huo umefanykak nyumbani kwa Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Halmashauri Kuu ya CCM imekutana leo chini ya mwenyekiti wake Dkt. John Magufuli na kumchagua John Pallangyo kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, lililoachwa wazi baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge wa jimbo hilo Joshua Nasari (Chadema) kwa kutoshiriki mikutano mitatu ya Bunge bila ruhusa yake.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza uchaguzi mdogo katika jimbo hilo baada ya kupokea barua ya Spika Ndugai.

TCRA yavilima vituo viwili vya redio kwa kusoma kwa kina habari za magazeti
Video: Kopafasta yazinduliwa rasmi nchini

Comments

comments