Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Desemba 5, 2018, amemtembelea na kumjulia hali Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Kumjulia hali, Rais Dkt. John Magufuli ameshiriki dua ya kumuombea Afya Njema iliyoongozwa na familia ya Rais huyo mstaafu.

Aidha, walioshiriki katika Dua hiyo Maalumu ni Rais Magufuli mwenyewe, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Bi. Sitti Mwinyi (Mke wa Mzee Mwinyi) pamoja na Abdallah Mwinyi (Mtoto wa Mzee Mwinyi).

Rais Magufuli ameiaga familia hiyo kwa kuwapa moyo kuwa mzee Mwinyi atarejea kwenye hali yake ya kawaida na kikubwa waendelee kumuombea tu.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 6, 2018
Msinililie mimi bali daini tume huru ya uchaguzi- Mbowe