Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko katika safu ya Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa kwa kuteua, kupandisha vyeo na kuhamisha vituo vya kazi.

Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi  imesema kuwa Rais Dkt. Magufuli ameteua na amewapandisha vyeo Naibu Makatibu Wakuu 4 na kuwa Makatibu Wakuu wapya na ameteua Naibu Makatibu Wakuu wapya 7 na wengine kuhamishiwa katika vituo mbalimbali vya kazi.

Aidha katika nafasi ya manaibu wapya waliopata nafasi ni pamoja na aliyekuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Thomas Kashillilah ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Stephen kigaigai, sasa amekuwa Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo.

 

  1. Ofisi ya Rais Ikulu.
  • Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata

 

  1. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  • Katibu Mkuu (Utumishi) – Laurian Ndumbaro
  • Naibu Katibu Mkuu – Dorothy Mwaluko

 

  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  • Katibu Mkuu – Mhandisi Mussa Iyombe
  • Naibu Katibu Mkuu(Afya) – Dkt. Zainabu Chaula
  • Naibu Katibu Mkuu(Elimu) – Bw. Tixon Nzunda
  1. Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
  • Katibu Mkuu – Mhandisi Joseph Kizito Malongo
  • Naibu Katibu Mkuu – Bi. Butamo Kasuka Phillipo

 

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
  • Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
  • Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) – Maimuna Tarishi
  • Katibu Mkuu(Sera na Uratibu) – Prof. Faustine Kamuzora

 

  1. Wizara ya Kilimo.
  • Katibu Mkuu – Mhandisi Methew Mtigumwe
  • Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Thomas Didimu Kashililah

 

  1. Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
  • Katibu Mkuu (Mifugo) – Dkt. Maria Mashingo
  • Katibu Mkuu (Uvuvi) – Dkt. Yohana Budeba

 

  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
  • Katibu Mkuu (Ujenzi) – Mhandisi Joseph Nyamuhanga
  • Katibu Mkuu (Uchukuzi) – Dkt. Leonard Chamriho
  • Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria Sassabo
  • Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina Madete

 

  1. Wizara ya Fedha na Mipango.
  • Katibu Mkuu – Doto James Mgosha
  • Naibu Katibu Mkuu (Utawala) – Bi. Susana Mkapa
  • Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina Shaaban
  • Naibu Katibu Mkuu (Sera) – Dkt. Khatibu Kazungu

 

  1. Wizara ya Nishati.
  • Katibu Mkuu – Dkt. Hamis Mwinyimvua

 

  1. Wizara ya Madini.
  • Katibu Mkuu – Prof. Simon S. Msanjila

 

  1. Wizara ya Katiba na Sheria.
  • Katibu Mkuu – Prof. Sifuni Mchome
  • Naibu Katibu Mkuu – Amon Mpanju

 

  1. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  • Katibu Mkuu – Prof. Adolf F. Mkenda
  • Naibu Katibu Mkuu – Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi

 

  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
  • Katibu Mkuu – Dkt. Florence Turuka
  • Naibu Katibu Mkuu – Bi. Immaculate Peter Ngwale

 

  1. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  • Katibu Mkuu – Meja Jen. Projest A. Rwegasira
  • Naibu Katibu Mkuu – Balozi Hassan Simba Yahaya

 

  1. Wizara ya Maliasili na Utalii.
  • Katibu Mkuu – Meja Jen. Gaudence S. Milanzi
  • Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Aloyce K. Nzuki

 

  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Katibu Mkuu – Dorothy Mwanyika
  • Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Moses M. Kusiluka

 

  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
  • Katibu Mkuu – Prof. Elisante Ole Gabriel
  • Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye
  • Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija

 

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
  • Katibu Mkuu – Dkt. Leonard Akwilapo
  • Naibu Katibu Mkuu – Prof. James Epiphan Mdoe
  • Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Ave-Maria Semakafu

 

  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
  • Katibu Mkuu (Afya) – Dkt. Mpoki Ulisubisya
  • Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) – Bi. Sihaba Nkinga.

 

  1. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  • Katibu Mkuu – Bi. Suzan Paul Mlawi
  • Naibu Katibu Mkuu – Nicholaus B. William

 

  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
  • Katibu Mkuu – Prof. Kitila Mkumbo
  • Naibu Katibu Mkuu – Mhandisi Emmanuel Kalobelo

Dkt. Kigwangallah apiga marufuku kamata kamata Pori Tengefu
Korea Kaskazini yaiachia Meli ya Korea Kusini