Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua spika mstaafu, Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Zakia Meghji kuwa Mwenyekiti wa Braza la chuo hicho.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo umeanza Disemba 6, 2018, ambapo mbali na hao Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo wenyeviti na wakurugenzi.

“Rais amemteua Prof. Esnati Osinde Chaggu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samwel Gwamaka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC,” imesema taarifa hiyo

Pia rais amemteua Meja Jenerali mstaafu, Michael Isamuhyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Profesa Gaspar Mhinzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA).

TCAA yajipanga kufanya majaribio ya mfumo wa Rada
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 7, 2018