Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania-IGP Simon Sirro kwa kuhakikisha watuhumiwa wote wa Dhahabu ya mamilioni ya pesa iliyokuwa inatoroshwa jijini Mwanza wamekamatwa wakiwemo Askari polisi 8.

Ametoa pongezi hizo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri na makatibu wakuu mbalimbali aliowateua.

Amesema kuwa watuhuhiwa hao walikamatwa January 4 Misungwi, kisha wakarudishwa kituo kikuu cha kati, lakini hawakuwekwa Mahabusu.

”Kwa taarifa nilizonazo, watuhumiwa wale walishikwa Januari 4, wilayani Misungwi, wakarudishwa mjini Mwanza na Kikosi cha Polisi nane, wakawapeleka Central wala hawakuwaingiza ndani, watuhumiwa walikuwa kwenye gari, wakawa wanajadili namna ya kuwapa hela, wakawaambia watawapa Bilioni 1,”amesema Rais Magufuli

Aidha, amesema kuwa watuhumiwa hao walitoa rushwa ya milioni 700, ikawa imebaki milioni 300 ambayo polisi hao waliahidiwa kwamba watapewa wakifika Sengerema.

Hata hivyo, rais Magufuli ameongeza kuwa baada ya kumfikia taarifa za kiintelijensia, akatoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwamba watu hao wafuatiliwe haraka na wakamatwe.

 

Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya Bavicha Serengeti
Cheka afunguka uchawi kwenye ndondi