Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Rais Magufuli amefanya uteuzi huo leo Novemba 18, 2016.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msingwa amesema pia Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi  katika Taasisi tano za Serikali ambapo Novemba 16, 2016 amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Novemba 17, 2016 amemteua Dk. Jones Kilimbe kuwa Mwenyekiti Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Makamu Mwenyekiti wake ameteuliwa Sylvester Mabumba, Novemba 17, 2016 Rais amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi  wa Taaisis ya Utafiti wa Vinatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI).

Amesema Novemba 16, 2016 Rais Magufuli pia amemteua Prof. Patrick Makungu  kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TENDO), Pia amemteua Martin Madekwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia na Ardhi, uteuzi huu umefanyika Novemba 17, 2016.

Mikel John Obi Kukimbilia Ufaransa, China
Samuel Afful: Subirini Moto, Tutakua Tishio