Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amenteua Profesa Lawrence Mujungu Museru kuwa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Oktoba 3, 2016 na katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Ikulu jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa uteuzi huo umeanza jana Oktoba 2, 2016.

Prof. Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli.

TANESCO Dodoma yaomba kupewa hadhi ya mkoa maalum
Video: Kamanda Sirro aeleza walivyomzima kibaka mtoboa macho