Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magufuli leo tarehe 11 julai, 2017 amefanya uteuzi na kumteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Prof. Florens D.A.M Luoga amechukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa.

Prof. Florens D.A.M Luoga ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Taaluma).

Ndege ya jeshi la Marekani yaanguka na kuua 16
Magazeti ya Tanzania leo Julai 11, 2017