Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo, Mei 16, 2020 ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli amemteu Dkt. Godwin Oloyce Mollel (Mbunge wa Siha) kuchukua nafasi hiyo.

Dkt. Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni aliteuliwa Oktoba 2017 kushika nafasi hiyo.

Dkt. Ndugulile aeleza alivyoupokea uamuzi wa Rais Magufuli, amuahidi Dkt. Mollel
Frank Lampard ashtuka

Comments

comments