Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua, Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Bashungwa anachukua nafasi ya aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Joseph George Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa, ambapo kabla ya uteuzi huo, Bashungwa alikuwa Naibu waziri wa Kilimo.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua, Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), akichukua nafasi ya Charles Edward Kichere ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha, kabla ya uteuzi huo, Mhede alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, ambapo uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda utafanywa hapo Baadaye.

Kufuatia uamuzi huo, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Erick Shitindi ambaye amestaafu.

China na Urusi zatema matumizi ya Dola
Video: Kishindo cha Magufuli kwa wafanyabiashara, PM aeleza maofisa wa TRA walivyodai rushwa