Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameishukuru serikali ya watu wa China kwa msaada wao walioutoa kwa wananchi wa Tanzania wa kuwapatia matibabu bure.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea meli yenye madaktari bingwa kutoka China ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma za vipimo na matibabu kwa wananchi bila gharama yoyote.

“Ninatoa shukrani za dhati kwa serikali ya China kuamua kuituma meli na madaktari kuja Tanzania, tunafurahi kwa huduma zao, wameokoa maisha ya watanzania zaidi ya elfu 6,400, huu ni upendo wa pekee unaogusa, ndio maana leo nimeshindwa kuvumilia nimeona bora nije nishukuru, nimeguswa mno na ndugu zetu wachina, yapo mataifa mengine matajiri, yenye mali nyingi lakini hayajaguswa”, amesema Rais Dkt. Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amewakabidhi madaktari hao barua maalum kwenda kwa raisi wa China Xi Jinping pamoja na kinyago kama zawadi kwake, kumshukuru kwa mchango wake na ukarimu wake kwa watanzania masikini.

 

Kiongozi wa ACT- Wazalendo aswekwa rumande
Mgombea wa Chadema awekwa chini ya ulinzi