Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu anatarajia kuhamia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma kama ilivyokuwa matamanio ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokwenda kumtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ambapo kabla ya kufika kwake alitumia fursa hiyo kushiriki nae ibada katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay.

“Azimio la Arusha ukilisoma unajua kila kitu kuhusu nchi yetu, baba wa taifa mwaka 1973 alisema tuhamie Dodoma ndio makao makuu ya nchi, Dodoma tunahamia na mimi ndio nakaribia kumalizia, mwezi wa 12 nihamie huko.”amesema rais Magufuli

Aidha, kitaifa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imefanyika Mkoani Tanga, ambapo wananchi wamejitokeza na kushuhudia sherehe hizo ambazo Mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar, Dkt. Ally Mohamed Shein

Hata hivyo, Oktoba 14 ndio tarehe ambayo Watanzania huwa tunaadhimisha kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambacho kilitokea mwaka 1999 baada ya kuugua kwa muda nchini Uingereza.

Trump aingilia kati sakata la kutoweka kwa mwandishi wa habari
Video: Rais Magufuli, Mkewe wamtembelea Mama Maria Nyerere