Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, John Pombe Magufuli leo Januari 17, 2018 amepiga marufuku michango ya aina yeyote inayochangishwa na walimu katika shule za zinazomilikiwa na Serikali za msingi na Sekondari.

Kupitia katazo hilo amewaagiza viongozi wa eneo hilo husika ambao ni Waziri wa Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali  za Mitaa (TAMISEMI), Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Ufundi Joyce L. Ndalichako kusimamia swala hilo ipasavyo.

Magufuli amepiga marufuku hiyo leo alipokutana na viongozi hao Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka kwenda kusimamia jambo hilo na kuhakikisha hakuna michango yoyote wanafunzi au wazazi wanachangishwa kwenye shule za sekondari na msingi ambazo zipo chini ya serikali.

 

Daktari wa Ikulu Marekani atoa taarifa za uchunguzi akili ya Rais Trump
Kingwangalla: Wasichana warembo na wakaka watanashati kuajiriwa