Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Magereza (CP) Dk. Juma A. Malewa kuwa Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini hadi hapo uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza utakapofanyika.

Hatua hiyo ni baada ya Rais Magufuli kukubali na kuridhia ombi la kusitisha mkataba na kustaafu kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP), John Casmir Minja kuanzia leo Desemba 2, 2016.

Rais Magufuli amempongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu John Casmir Minja kwa utumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu.

Video: Makonda afanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi ofisi za bakwata
Serikali yapiga marufuku uchapaji holela wa vitabu