Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa anatamani kabla ya kumaliza muda wake kuwe na mabilionea 100 Watanzania.

Ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Hadi sasa, Tanzania ina bilionea mmoja kwa mujibu wa Jarida la Forbes. Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji ambaye ni mfadhili mkuu wa Klabu ya Simba anatajwa kuwa mmoja kati ya mabilionea wachache barani Afrika akiwa na utajiri wa $1.9 bilioni (sawa na Sh. 4.37 trilioni za Kitanzania).

Aidha, Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu wakati Serikali ikiendelea kuhakikisha inawatengenezea mazingira bora zaidi.

”Nawaomba sana ndugu zangu Wafanyabiashara tulipe kodi, tusikwepe kulipa kodi tuwe waaminifu, natamani sana kumaliza muda wangu nikiwa na mabilionea mia moja kutoka Tanzania, hii ni kiu yangu kubwa sana,”amesema Rais Magufuli.

Aidha, amesema kuwa ana taarifa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamejenga viwanda kama geresha na wanatumia viwanda hivyo kupokelea au kutunzia bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi stahiki.

Lugola awavutia upepo Polisi kuhusu bodaboda, ‘hawatajua siku wala saa’
LIVE IKULU: Rais Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara leo Juni 7, 2019

Comments

comments