Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Julius Ndyamukana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Mhandisi Ndyamukana anachukua nafasi ya Richard Mayongela ambaye uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambako atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Ndyamukana alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Dar es salaam ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa majengo namba 3 (Terminal 3) ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Dar es salaam ambayo yapo hatua za mwisho kukamilika.

Katika taarifa hiyo, imesema kuwa uteuzi wa Mhandisi Ndyamukana unaanza leo tarehe 26, 2019.

NEC yaanza maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2020
Zifahamu faida muhimu za asali,

Comments

comments