Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Mohamed Maja kuanzia leo kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuisababishia halmashauri hiyo upotevu mkubwa wa fedha za serikali.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mussa Iyombe wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo amesema kuwa utenguzi huo umefanyika ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

Amesema kuwa tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa utendaji katika ofisi ya mkurugenzi huyo imebaini baadhi ya fedha zinapotea mikononi mwa watu na mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege amewataka wenyeviti wa halmashauri kote nchini kuzingatia mafunzo waliyopewa na uongozi wa chuo cha serikali za mitaa hombolo ili wawe mabalozi bora katika maeneo yao.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 7, 2018
Mbao FC waendelea kupumulia mashine

Comments

comments