Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti saba  wa Bodi na Taasisi za Serikali, na pia amemteua Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji  wananchi Kiuchumi Tanzania na mjumbe mmoja wa Baraza la Taifa la Biashara.

Aidha taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imewataja walioteuliwa kuwa ni Kisare Makori, ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo akichukua nafasi ya Humphrey Pole pole, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi.

Pia Rais Magufuli amemteua Avod Mmanda, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara akichukua nafasi Dkt. Khatibu Kazungu ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mbali na hilo amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri ambapo Ramadhan Mwangulumbi, ameteuliwa kuwa DED wa Manispaa ya Shinyanga kuziba nafasi iliyoachwa wazi na  Lewis Kalinjuna ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Rais Magufuli amemteua Rashid Gembe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga liyopo Tanga na kuongeza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja na wateule wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Video: JPM atumbua vigogo 300, Faru John sasa 'kufa' na vigogo....
Melo aachiwa kwa dhamana