Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kauli yake kama mkuu wa nchi juu ya kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi siku ya Februari 16 mwaka huu.

Aidha, kwenye ukurasa wake wa twitter Rais Dkt. Magufuli ameandika ujumbe kuhusu kusikitishwa kwake na kifo cha Akwilina, na kuagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatu waliohusika.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).Natoa pole kwa familia,ndugu, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili”, ameandika rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Akwilina alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji jijini Dar es salaam, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa vurugu za siasa zilizotokea siku ya Ijumaa, akiwa kwenye daladala.

Polisi yatoboa siri ya mauaji kada wa Chadema
Majeshi ya Congo DR na Rwanda yashambuliana