Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya biashara yake

Ametoa agizo hilo mapema hii leo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.

Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi hivyo ninato siku kumi na nne, wakishindwa wafutiwe leseni, amesema Rais Magufuli

Aidha, katika hatua nyingine Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine kwani kufanya hivyo ni kuongeza gharama za usafirishaji zisizo umuhimu wowote.

Manji azidi kusota Gerezani, sasa aanza kupatiwa matibabu huko huko
Lucas Leiva Atambulisha SS Lazio