Rais Dkt. John Magufuli ametoa siku saba kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi kuhakikisha anakamilisha zoezi la kufuta hati za umiliki wa ardhi Kilosa mkoani Morogoro kwa mtu asiye na uraia wa Tanzania.

Hayo yamejiri baada ya Waziri Lukuvi kufafanua juu ya mashamba ya hekta 5000 aliyomilikishwa raia wa China ambayo Rais alitoa maagizo wagawiwe wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi wilayani humo.

“Sheria ya matumizi ya ardhi ya mwaka 2007, ni kwamba ardhi yeyote Tanzania haiwezi ikamilikishwa na mtu ambaye si mtanzania, inamilikishwa kwa mtu ambaye si mtanzania kama amepitia TIC kwajili ya uwekezaji” amesema Magufuli.

Na kusisitiza “Watanzania wanakuwa watumwa kwenye nchi yao, Sasa maagizo yangu ni haya, ndani ya wiki moja iletwe hiyo hati, zikatwe hekta flani wagawiwe wananchi wa hapa Kimamba”.

Aidha ametoa agizo kwa wananchi baada ya kuyagawa hayo mashamba kwa wafugaji na wakulima wahakikishe kila mtu anapata na isiwe chanzo cha migogoro mingine kwani wakulima na wafugaji wanategemeana.

Serikali yabainisha wanafunzi wasiotakiwa kuvaa barakoa
Trump atupiwa lawama kampeni na ubaguzi wa rangi