Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Agness Gerald Waya kufuatia kifo cha mtoto wao Agness alimaarufu kama Masogange kilichotokea Ijumaa.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM, Kheri James na kusema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha binti huyo kwani kifo chake kinapunguza idadi ya vijana ambao ndiyo jeshi na watu ambao wanaweza kufikisha mbali taifa.

“Kupitia jukwaa hili naomba nitoa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye leo amewasilisi mjini Dodoma lakini ameomba niwasilishe kwenu salamu za pole kwa kuondokewa na kijana mwenzetu, Mwenyekiti anafahamu nchii hii sisi vijana ndiyo warithi wa taifa hili sisi ndiyo tumebeba dira ya kulifikisha taifa ambapo tunadhani linafaa kufika hivyo anasikitishwa sana kuona katika jeshi kubwa kama hili la vijana tunapungukiwa na vijana wenzetu wanaondoka na kupunguza idadi ya askari wetu, naomba mpokee salamu za Mwenyekiti wetu,” amesema Kheri James 

Hata hivyo Mwili wa Agness Masogange utazikwa jijini Mbeya nyumbani kwa wazazi wake alipoza Mbalizi jijini humo

 

 

Video: Salamu za Diamond, Alikiba msiba wa Masogange
ACT yasitisha mkutano kwa sababu za kiusalama