Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo iliyotokea mpakani mwa Mkoa wa Songwe na Mbeya na kusababisha vifo vya watu vya watu 19.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali mstaafu, Nicodemas Mwangela kufikisha salamu zake za pole.

Aidha imeeleza kuwa Rais Magufuli amezitaka mamlaka zinazohusika na usalama wa barabarani mkoani Songwe kufanya uchunguzi wa ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili.

Ajali hiyo imetokea usiku wakuamkia leo majira ya saa 3 usiku katika eneo lenye mwinuko mkali katikati ya mpaka wa Mbeya na Mkoa wa Songwe ambapo mpaka sasa jeshi linaendelea kuhakikisha barabara ya sehemu ajali ilipotokea inaweza kupitika vizuri.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando amesema kuwa ajali hiyo iliyoua watu 19 baada ya kutokea imehusisha gari aina ya Lori namba T 825 CMJ lililoigonga gari yenye nambari T 269 CJC aina ya Coaster.

 

Simba yaendelea kutakata, yailamba Azam FC 3-1
Serikali kudhibiti taasisi binafsi na mashirika ya dini