Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaalika Ikulu wafanyabiashara wakubwa kutoka wilaya zote nchini, kwa lengo la kuzungumza nao.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Juni 7 katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa barua ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo aliyowaandikia wakuu wote wa mikoa, kila wilaya inapaswa kuwakilishwa na wafanyabiashara watano wakubwa zaidi.

Barua hiyo imeeleza kuwa orodha hiyo ya majina ya watakaochaguliwa inapaswa kuambatana na aina ya biashara wanayofanya pamoja na namba zao za simu.

Ujumbe ulio kwenye barua hiyo unawasisitiza wakuu hao wa mikoa kutosita kuwajumuisha wanasiasa na wafanyakazi wa serikali ambao wanaendesha biashara kubwa.

Rais Magufuli amekuwa akikutana na makundi mbalimbali Ikulu na kujadili nao masuala yanayohusu sekta au maeneo wanayofanyia kazi. Ameshakutana na wafanyabiashara ya madini na viongozi wa dini.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 4, 2019
Jay Z awa rapa wa kwanza kuwa bilionea