Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho katika mkutano mkuu wa NEC uliofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Wanachama hao ambao wamehamia na kutangazwa ni Mwanasheria, Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo, Mbunge wa zamani wa Nyamagana Lawrence Masha aliyekuwa mwanachama wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa Chadema taifa, Patrobas Katambi.

Aidha, wengine ni Prof. Kitila Mkumbo ambaye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa muda.

“Nawaomba msije mkabadilika tena, mmekuja huku na wanachama wamewakubali msirudi tena kule, hiki ni chama cha wote hata watoto watazaliwa watakikuta na watajiunga kwasababu kina misingi imara, kwa hiyo msije huku kujaribu,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amewapa ruhusa ya kugombea nyadhifa mbalinmbali ndani ya chama na kwenye maeneo yao ili kuimarisha demokrasia ndani ya chama hicho..

 

Grassroots yafanyika kwa mafanikio Lindi
Sofia Simba arejeshwa CCM, aomba radhi kwa usaliti