Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Shirikisho la Taifa la Utengenezaji wa Mitambo ya Viwanda la China (CNMIF) kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawapa ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme, viwanda na kilimo hapa nchini.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF na Mbunge wa Bunge la Wananchi wa China, Zhan Xin.

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Megawatts kati ya 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia Megawatts 10,000 na kwamba ili kufikia malengo hayo, wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama vile gesi, makaa ya mawe na jua.

Rais Magufuli pia amekutana na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Malika Berak ambapo viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa mambo mbalimbali ya ushirikiano pamoja na miradi ya maendeleo iliyotokana na makubaliano ya Mkutano wa wafanyabishara wa Tanzania n aUfaransa uliofanyika hivi karibuni.

Pia, Rais Magufuli amekutana na viongozi wengine na kufanya mazungumzo; Kaimu Balozi wa Uturuki hapa nchini, Yunus Belet na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Korea, Songwon Shin.

Video: Mrema awaonya wanaomkosoa JPM
Manji athibitisha kujiuzulu Yanga