Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali na kumteua Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Mpambe wa Rais (Aide de Camp – ADC).

Katika taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam imesema kuwa Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.

Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1 kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.

 

Nicki Minaj kushusha vyuma viwili leo, aonjesha kishindo
Joshua, Wilder watishiana bei kuvunja rekodi ya masumbwi

Comments

comments