Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa anashangazwa na vikundi vya watu wachache vilivyopo nchini wakizungumzia kero zinazohusu masuala ya viwanda wakati wao wenyewe hawana hata kiwanda cha Pipi.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 11 unaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya biashara nchini, na namna ya kutatua changamoto zinazoikwamisha sekta hiyo kuendelea kukua na kupanuka kimataifa zaidi.

“tangu baraza hili lianze kumekuwa na kundi fulani la watu wachache na wengine hata hawana viwanda lakini wanazungumzia viwanda, unamkuta mtu hana kiwanda hata cha pipi lakini kila siku anazungumzia kiwanda ndio maana nikaamua nyie wenye viwanda ambao mnazipata hizo changamoto tujue tatizo ni nini ili serikali iweze kujua chakufanya,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka serikalini pamoja na wafanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa IPP Reginald Mengi, Mohamed Dewji ‘MO’, Said Salim Bakhresa na wengine wengi

Bocco awatuliza mashabiki wa Simba
TFF yafafanua kuhusu matumizi ya bilioni 3.7